NORTH MARA – Pande 3 Za Uwajibikaji
Tumekuwa na mengi ya kujadili na kutolea maoni kuhusu suala Tata la Mgodi wa North Mara haswa Suala la Mto Tigithe mambo haya kwa namna moja ua nyingine yametokea kufaidisha wale ambao walitoa habari hiyo kwa mara ya kwanza na kuifanyia biashara kama haya mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs ambayo yalitumia Habari hii kuombea misaada na aina nyingine ya vitu kwa ajili ya kazi zao mbalimbali .
Kuna wananchi ambao wengi wao ndio wanalishwa habari hizi haswa wale waliosoma habari na picha za matukio haya kupitia vyombo mbalimbali vya habari haswa tovuti na blogu mbalimbali popote walipo duniani hawa wamekuwa ndio wakutupiwa kila kilichokibaya na hujuma dhidi ya north mara muda wote lakini vile vizuri wananchi hawa hawana haki ya kujua au hata wakijaribu kujua basi wanatakiwa kazi ya ziada .
Pia kuna kampuni ambayo imewekeza katika eneo hilo kampuni zote kuanzia east African minerals mpaka placerdome na sasa African Barrick Gold zote hizo zimefanyakazi kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati yake na wananchi wa maeneo hayo ambayo ndio wamiliki wa ardhi , serikali ambaye ndio msimamizi na mtunga sera na mkaribishaji na vyombo vingine ambavyo kwa namna moja au nyingine vinahusika na suala la uendeshaji wa North Mara .
Mkubwa kuliko wote ni serikali na ambayo ndio wenye mamlaka yote kwenye eneo hilo wao ndio wasimamizi wakuu wao ndio walio kati kati ya wananchi na north mara wao ndio wanatakiwa kuwa wasemaji wa mwisho baada ya kuona habari mbalimbali kuzitolea ufafanuzi na kuwapa wananchi na wengine waliokuwa wanataka taarifa hizo lakini serikali inafanya pale ambapo mkono wake unafikia ila pale ambapo kuna mgongano wa kimaslahi haswa katika masuala ya kisiasa serikali huwa makini zaidi katika kushugulikia suala kama hilo isije kupoteza imani kwa wananchi , isije kukosa imani kwa kampuni za uwekezaji na yenyewe isije kuleta migongano kati ya wafanyakazi wake .
Mimi ni niko kwenye kundi la wananchi ambao kwa kiasi kikubwa tulipotoshwa na habari zilizosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari haswa tovuti na blogu kuhusu kile kilichokuwa kinafanyika na kuendelea kwenye mgodi wa north mara hata wewe kama ulisoma na kuona habari hizi bila kujua hali halisi unaweza kupata hasira na hata kuchukuwa hatua zingine .
Nilifika eneo la mto tigite na maeneo mengine North mara na kujionea masuala na mambo mengine mbalimbali ya kijamii kuna maeneo ambayo yamehujumiwa na kampuni ya African Barrick Gold imeingia hasara kubwa katika kurekebisha hali hiyo lakini bado wananchi wameendelea kuhujumu miundombinu hiyo kwa sababu zisizoeleweka kabisa .
Tukiongelea uhujumu wa miundo mbinu ni pale kampuni ya ABG inapokuwa imeweka carpet kwenye mabwawa ya kuhifadhi maji taka lakini wananchi hao wanakata carpet hizo na kwenda kuzitumia kwenye shuguli zao mbalimbali kama kuezeka nyumba kwa sababu ya ugumu wake na hata kuuziana wenyewe mitaani sasa yale maji taka yenye sumu huingia kwenye ardhi moja kwa moja na kusafiri pale mvua zinaponyesha kwenda kwenye mikondo ya maji matokeo yake tunayajua ni maafa .
Wakati ambapo ABG inapojaribu kuweka mashimo kwa ajili ya kupima uchafuzi wa mazingira au kukusanya taarifa zingine za mazingira maeneo hayo wananchi wanaamua kuingiza mawe kwenye vifaa vilivyowekwa kwenye mashimo hayo , wananchi hao hao hukata mabomba ya maji yanayosafirisha uchafu kupeleka kwenye mabwawa .
Pili ni wachimbaji wadogo wadogo wanapojaribu kuchuja mchanga wenye madini kutumia marigafi zingine kando kando ya mito kisha kuacha sumu hiyo kuingia kwenye maji mvua inaponyesha ile sumu husafiri kufuata mkondo wa maji yale wakati hii ikiendelea serikali inajua kwamba kuna wachimbaji wadogo wadogo wanaofanya hivyo pembeni ya mito na vyanzo vingine vya maji ambavyo watu hutumia kwa ajili ya shuguli zao za kila siku .
Ninapoongelea pande tatu ya uwajibikaji naongelea ABG kuwajibika ambapo imekuwa ikifanya hivyo kwa kiwango kikubwa kwa sababu ina uwezo , wataalamu na vifaa na ni sehemu ya vijiji 8 vya eneo la north mara – SERIKALI ambayo ndio mkuu wa eneo hilo linalotoa leseni na vibali vya kufanya kazi kwa ABG na Wachimbaji wadogo na ambayo huchukuwa kodi toka kwa sehemu zote hata kuchukuwa taarifa za hali ya mazingira na zingine kwenye eneo hilo – WANANCHI ambao ndio wamekutwa eneo hilo na ambao wanafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na uwekezaji huo lakini wanaoamua kukaribisha wageni na magenge mengine ya kihuni kuharibu miundo mbinu na aina zingine za hujuma kwa kuendeleza tabia za rushwa na ujeuri .
NI VIZURI KILA MTU ACHUKUWE UPANDE WAKE WA KUWAJIBIKA HUKU AKIHAKIKISHA HAKUNA ANAYEPOTEZA HAKI ZAKE AU KUPOTEZA IMANI KATI YA PANDE MOJA NA NYINGINE .
NIMETEMBELEA NIMEONA – NANYI TEMBELEENI MUONE MSIKUBALI KUDANGANYIKA HII NI NCHI YETU WOTE NI WAJIBU WETU KUTETEA MASLAHI YAKE .
--You received this message because you are subscribed to the "USA-Africa Dialogue Series" moderated by Toyin Falola, University of Texas at Austin.
For current archives, visit http://groups.google.com/group/USAAfricaDialogue
For previous archives, visit http://www.utexas.edu/conferences/africa/ads/index.html
To post to this group, send an email to USAAfricaDialogue@googlegroups.com
To unsubscribe from this group, send an email to USAAfricaDialogue-
unsubscribe@googlegroups.com
No comments:
Post a Comment